Idara ya shule za wasichana za Alkafeel inafanya maonyesho ya wanawake ya hati na mapambo ya kisanii…

Maoni katika picha
Idara ya shule za wasichana Alkafeel ambazo zipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya maonyesho ya hati na mapambo ya kisanii ya kazi za wanawake, ndani ya jengo la kituo cha Swidiiqah Twahirah (a.s), yakiwa ni miongoni mwa shughuli za kongamano la kitamaduni na kimataifa Ruhu Nubuwa awamu ya tatu, kwa kushiriki idadi kubwa ya wanafunzi wa shule za Alkafeel pamoja na wasichana walioshiriki katika mashindano maalumu yaliyoa andaliwa kwa ajili ya kongamano hili.

Maonyesho haya yalifunguliwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), maonyesho yamepambwa na vitu mbalimbali, kuna: mbao za kisanii, hati, kazi za mikono na picha za mnato.

Kuhusu maonyesho haya tumeongea na Ustadhat Bushra Kinani ambaye ni kiongozi wa shule za wasichana za Alkafeel, amesema kua: “Maonyesho ya kazi za Sanaa ni moja kati ya ratiba muhimu za kongamano, maonyesho haya yamependeza kushinda maonyesho yaliyo pita kutokana na kuhusisha watu wa rika zote, wote wamefanya vizuri katika nafasi zao za ushiriki, maonyesho yamegawika sehemu nne, sehemu maalumu ya hati za kiarabu na mapambo ya kiislamu, na sehemu ya fani mbalimbali na mapambo na sehemu ya kazi za mikono”.

Akaongeza kua: “Kuhusu mashindano tulikua na washiriki wa kila fani, kazi zilizo tumwa kushiriki mashindano tulizikabidhi kwa kamati maalumu ya watalaamu (majaji) kwa ajili ya kuzichuja, kamati hiyo ilikua na masharti ya kushiriki katika mashindano, miongoni mwa masharti hayo ni: kuheshimu mazingira ya wasimamizi wa mashindano na kauli mbiu ya kongamano, kamati iliandaa zawadi za washindi katika kila aina ya shindano, pamoja na vyeti vya ushiriki ambavyo anapewa kila mshiriki, washindi watatu wa mwanzo walikua hawa wafuatao:

  • - Zaharaa Abbasi Khadhwiir kutoka Iraq, mshindi wa ubao bora zaidi wa kisanii.
  • - Hindi Sajjaad Mussawi kutoka Iraq, mshindi wa picha bora zaidi ya mnato.
  • - Azhaar Sharikaau rais wa muungano wa wanahati kutoka Jamhuri ya kiislamu ya Iran, mshindi wa ubao bora zaidi wa hati”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: