Marjaa dini mkuu amelaani vikali jinai zilizo fanywa na magaidi wa Daesh hivi karibuni na ametangaza kuungana na watu wa kabila la Aizidiy…

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amelaani vikali jinai zilizo fanywa na magaidi wa Daesh katika mji wa Najafu na Tharthaar, na ametangaza kuungana na watu wa kabila la Aizidiy kutokana na udhalilishaji mkubwa walio fanyiwa mabinti zao ikiwa ni pamoja na kuwawa na kusulubiwa miili yao kwa kukatwa vichwa, akasema kua huo ni unyama wa kutisha ambao ni nadra kutokea katika dunia ya leo.

Ameyasema hayo kupitia mwakilishi wake Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai (d.i) katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyoa swaliwa ndani ya uwanja wa haram ya Imamu Hussein (a.s) leo (23 Jamadal Thani 1440h) sawa na (01 Machi 2019m), ifuatayo ni nakala ya tamko lake:

Nataka kuzungumzia jinai za kutisha zilizo ripotiwa na vyombo vya habari hivi karibuni, kupatikana miili hamsini ya wasichana wa Aizidiy iliyobakwa na kukatwa vichwa na magaidi wa Daesh, sioni maneno ya kuelezea unyama huu ambao ni nadra kutokea duniani, tunatangaza kushikamana na ndugu zetu raia wa Iraq pamoja na taasisi za kimataifa na kutaka ufanyike uchunguzi wa jinai hizo za magaidi wa Daesh, na kuhakikisha wahusika wote wanakamatwa na kuhukumiwa, hali kadhalika siku za hivi karibuni magaidi wa Daesh wamefanya mashambulio mapya katika mji wa Najafu na kwenye jangwa na Nukhaibu na ziwa Tharthaar, na kupelekea kuuwawa kwa vijana wetu waliokua katika kazi za kawaida za kujitafutia riziki, tunaomba serikali ya Iraq ichukue tahadhari za makusudi na kuhakikisha matukio ya aina hii hayatokei tena, wanatakiwa washambuliwe magaidi wa Daesh popote walipo na kuhakikisha hawapati nafasi ya kufanya jinai zao sehemu yeyote katika taifa la Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: