Kuanza kwa hatua ya pili ya shindano la (Soma fanya ziara na umra)…

Maoni katika picha
Chini ya kauli mbiu: (Kutoka kwa Abulfadhil Abbasi huja utukufu) na kwa mwaka wa pili, Maahadi ya turathi za Mitume (a.s) ya masomo ya hauza kwa njia ya elektronik chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kuanza hatua ya pili ya shindano la (soma fanya ziara na umra) ambalo ni mradi wa kusoma juzuu moja la Quráni tukufu na kulizawadia kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa nia ya kukidhiwa haja na kupona wagonjwa.

Zawadi ya kushiriki katika shindano hili ni kufanya umra kwa niaba katika mwezi wa Rajabu na Shabani, na kufanya ziara kwa Mtume (s.a.w.w) na Maimamu wa Baqii (a.s) kwa niaba, inatakiwa kuzingatia yafuatayo:

  • 1- Niaba inasihi kwa waliohai na waliokufa.
  • 2- Atakaye shiriki kwa kusoma juzuu mbili atapewa zawadi yake na ya wazazi wake.
  • 3- Kuchagua kusoma juzuu moja tuma namba (1) na juzuu mbili tuma namba (2).
  • 4- Ukimaliza kusoma tuna neno (maliza).
  • 5- Niaba zinaidadi maalumu wahi nafasi.
  • 6- Kwa ajili ya kushiriki fuata maelekezo yafuatayo:
  • - Wanawake wajiandikishe kupitia anuani hii: mosabeqat_alasheqien_nesaa@. Na haifai kisheria wanaume kujiandikisha katika anuani hiyo.
  • - Wanaume wajiandikishe kupitia anuani hii: ashqain2@.
  • - Kujiandikisha kupitia ukurasa wa facebook ingia hapa:

https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=2292211597497958&id=1115686655150464

kumbuka kua Maahadi ya turathi za Mitume (a.s) kwa masomo ya hauza kielektronik ni moja ya taasisi za Atabatu Abbasiyya tukufu na inamalengo mengi, miongoni mwa malengo hayo ni:

  • 1- Kujenga uwelewa katika jamii na mafundisho ya Mwenyezi Mungu na tabia njema.
  • 2- Kushajihisha wanafunzi na watafiti kufanya tafiti mbalimbali na kuwapa mambo wanayo hitaji katika tafiti zao.
  • 3- Kusambaza elimu ya Ahlulbait (a.s) kwa wanaohitaji kila sehemu ya dunia, hususan elimu ya Dini kwa njia ya kielektronik ni rahisi kwa kila mtu, hasa wale ambao hawawezi kwenda Najafu kusoma, na kuandaa mubalighina katika miji tofauti, sambamba na kuandaa kizazi cha wasomi wenye uwezo wa kusambaza ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa watu tofauti, na kuandaa wakina mama wanaoweza kutoa malezi mema kwa watoto wao, hakika wao ndio huzaa majemedari.
  • 4- Kuongeza kiwango cha elimu ya mubalighina na viongozi wa Dini pamoja na kuhamasisha wafuasi wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: