Hospitali ya rufaa Alkafeel imesema kua milango yake iko wazi kwa kila anayetaka kupata huduma bora za afya na raia wa Iraq wanapewa kipaombele zaidi…

Maoni katika picha
Mkuu wa hospitali ya Alkafeel ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Muhammad Azizi, amesema kua milango ya hospitali iko wazi kwa kila anayetaka kupata huduma bora za afya na raia wa Iraq wanapewa kipaombele zaidi.

Ameyasema hayo katika ujumbe aliotoa kwenye ufunguzi wa warsha ya vitengo vya kukagua ubora vya mikoani, inayo simamiwa na baraza la mawaziri kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Karbala pamoja na hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya kauli mbiu isemayo: (Ubora ni jukumu la wote).

Akaongeza kua: “Tunafuraha kubwa kuhudhuria kwenu katika hospitali ya rufaa Alkafeel na tunawakaribisha sana, ni utukufu mkubwa kwetu kushiriki katika warsha hii ya ubora, hakika hili ni jambo jema na hatua tukufu katika kuboresha huduma za afya hapa Iraq, kwa kuwa kila kitu kinautaratibu na njia ya kukufikisha katika jambo unalo kusudia, hospitali ya rufaa Alkafeel imefungua milango yake kwa kila anayetaka kupata huduma bora za afya”.

Akabainisha kua: “Tumefikia vigezo vya ubora vinavyo kubalika na kila nchi kwenye utowaji wa huduma za afya, kutokana na dosari zilizo jitokeza na namna zilivyo tatuliwa, sisi katika hospitali ya rufaa Akafeel daima tumekua tukiangalia namna ya kuongeza ubora wa huduma zetu hadi ziendane na ubora wa kimataifa, hadi sasa hospitali yetu inafanya kazi kwa viwango vya ubora wa kimataifa katika kila sekta”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: