Kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada awamu ya kumi na tano yatangaza kuongeza muda wa kupokea tafiti za kongamano

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada awamu ya kumi na tano, imetangaza kuongeza muda wa kupokea tafiti zitakazo shiriki kwenye shindano la kongamano hadi tarehe (10 Rajabu 1440h), hapo awali mwisho wa kupokea tafiti hizo ilikua tarehe (1 Rajabu 1440h) sawa na (9 Machi 2019m).

Tumeongea na mjumbe wa kamati ya maandalizi Shekh Ammaar Hilali na rais wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, amesema kua: “Tumeongeza muda wa kupokea tafiti zitakazo shiriki kwenye shindano la kongamano baada ya kujadiliana kwa kamati ya maandalizi, pamoja na kuzingatia muda utakao tumiwa na jopo la majaji katika kuchuja tafiti hizo, kwa hiyo tumeongeza siku (9), mwisho wa kupokea tafiti utakua (10 Rajabu) sawa na (17 Machi 2019m)”.

Akaongeza kua: “Kuongeza muda kumetokana na maombo ya watafiti watakao shiriki katika kongamano, sambamba na kutowa nafasi ya kupotea tafiti nyingi Zaidi kwa kiasi itakavyo wezekana, vilevile kutokana na nafasi adim ya kuwakutanisha wachambuzi kutoka kila sehemu ya dunia, tafiti hizo ni zawadi ya kifikra na kitamaduni kwa kuwa zina mambo muhimu Zaidi”.

Kumbuka kua kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada huandaliwa na kusimamiwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya tangu kuanzishwa kwake, kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), litafanyika mwanzoni mwa mwezi wa Shabani (Insha-Allah) chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Hussein (a.s) ni mnara wa umma na mtengenezaji wa misingi)
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: