Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki katika kuandaa semina za kukuza vipaji vya mayatima wa mashahidi wa jeshi la serikali na Hashdi Shaábi

Maoni katika picha
Tangu ilipotolewa fatwa ya jihadi ya kujilinda Atabatu Abasiyya tukufu imekuwa moja ya taasisi zinazo fadhili jambo hilo, ufadhili wake umekua wa aina mbalimbali kutokana na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu, bado inaendelea kusaidia mayatima na wajane wa mashahidi wa fatwa hii tukufu, ambayo imeleta amani na utulivu kwa wairaq, kushiriki kwake katika kuratibu semina ya kubaini na kuendeleza vipaji vya mayatima ni moja ya muendelezo wa ufadhili wao kwa watu hawa.

Uratibu na uwendeshaji wa semina hii unafanyika kwa kushirikiana na Atabatu Husseiniyya pamoja na taasisi ya Answaru Fatuma Faharaa (a.s), umejikita katika kutoa masomo ya muda mfupi kuhusu namna ya kuendeleza vipaji vya mayatima, pamoja na njia za kutoa khutuba, huduma ya uwokozi ya kwanza, maelekezo ya kifamilia, uchoraji, upigaji wa picha, kujifundisha usomaji sahihi wa surat Fat-ha pamoja na mambo mengine mengi, semina hii ni miongoni mwa miradi ya kitaifa ya kusaidia na kukuza vipaji vya wairaq.

Fahamu kua semina hii ni mwendelezo wa shughuli nyingi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa familia hizi kutokana na namna walivyo jitolea katika kulinda taifa hili, na kuwafanya mayatima wasijihisi unyonge katika jamii kutokana na uyatima wao.

Kumbuka kua mradi huu ni miongoni mwa miradi ya kitaifa, unalenga kuinua vipaji vya mayatima wakiume na wakike pamoja na kusaidia familia za mashahidi kwa kushirikiana na taasisi za kijamii, ni mradi huru kwa unaofadhiliwa na muasisi wake pamoja na sadaka za baadhi ya wahisani, unalenga kuibua vipaji vya mayatima na kuviendeleza kwa kuwapa semina zinazo endana na vipaji vyao, sambamba na kuwatafutia kazi au mradi unaosimamiwa na wataalamu wetu, kwa ajili ya kuwafanya waweze kujitegemea na kupata maisha mazuri pamoja na familia zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: