Kwa kuhudhuria kiongozi mkuu wa kisheria: Atabatu Abbasiyya tukufu yatoa zawadi kwa familia za mashahidi wa Hashdi Shaábi

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu bado inawakumbuka mashahidi wa Iraq walio jitolea roho zao kwa ajili ya kulinda taifa na maeneo matukufu, kituo cha utamaduni wa familia chini ya Ataba tukufu kimetoa zawadi kwa familia za mashahidi wa Hashdi Shaábi, kwenye hafla iliyo fanyika ndani ya ukumbi mkuu wa kituo cha Swidiiqah Twahirah (a.s) alasiri ya Alkhamisi (29 Jamadal Thani 1440h), katika mnasaba wa kumaliza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa kituo hicho, na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi pamoja na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar sambamba na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi.

Wamepewa zawadi za aina mbalimbali, na miongoni mwa walikua wanakabidhi zawadi ni Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi.

Utowaji wa zahadi unatokana na mwenendo wa kituo hiki tangu kilipo anzishwa, katika shughuli zake huwa kinatenga nafasi maalumu kwa ajili ya familia za mashahidi wa jeshi la serikali na Hashdi Shaábi, kutokana na namna walivyo jitolea nafsi zao kwa ajili ya kulinda taifa na maeneo matukufu.

Familia za mashahidi zimetoa shukrani nyingi kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kituo cha utamaduni wa familia kwa kuwapa zawadi hizi, wakasema kua wao kupewa zawadi na Atabatu Abbasiyya sio jambo geni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: