Kikao cha mada za kitafiti cha kwanza kimefanyika ndani ya ukumbi wa Shekh Tusi kwenye jengo la taasisi (ya Bahrul Uluum Alkhairiyya) katika mkoa wa Najafu, hicho ni kikao cha kwanza katika vikao vinne vinavyo tarajiwa, vikao viwili vitakua hapa, na vingine viwili kwenye ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Kikao cha ufunguzi kiliongozwa na Dokta Hakim Habibu Kuraitwi na walioshiriki katika kuwasilisha mada za kitafiti ni:
- - Dokta Rahmani Gharkani, utafiti wake unasema: (Muhammad Bahrul Ulumi katika machapisho yake).
- - Dokta Ali Yusufu Nurudini, utafiti wake unasema: (Nafasi ya hauza ya Najafu katika kukihudumia kiarabu na wanachuoni wake mashuhuri wa zama hizi).
- - Dokta Hiyaam Abduzaidi, utafiti wake unasema: (Athari ya hauza katika harakati za kurekebisha lugha, Shekh Karbasi kama mfano).
- - Dokta Haidari Jabbari Idani Abu Swibii, utafiti wake unasema: (Somo la Nahau katika hauza, Shekh Muhammad Ali Mudarisi maarufu kwa (mwalimu wa kiafghani) wa mwaka 1329 – 1406h kama mfano).
- - Dokta Jaasim Farihi Daaikh Turabi, utafiti wake unasema: (Selebasi za lugha katika hauza .. masomo na mpangilio).
- - Ustadh Muhammad Ni’imah Samawi, utafiti wake unasema: (Najafu ni kitovu cha uboreshaji wa mashairi ya kiarabu.. Shekh Abdulhamidi Samawi kama mfano).
- - Dokta Swabahu Anuuz, utafiti wake unasema: (Mashairi ya Sayyid Muhammad Bahrul Uluum (r.a) baina ya misingi na visa katika uhalisia wa maisha).
Kikao hiki kilikua na mwitikio mkubwa kutokana na ubora wa tafiti zake kwani zimejikita katika mambo yaliyokua hayajazungumzwa sana, na kulikua na maoni, maswali na michango mbalimbali kutoka kwa wahudhuriaji, ambapo watafiti walijibu na kufafanua pale walipo hitajika kutoa ufafanuzi zaidi.