Miongoni mwa mfululizo wa nakala kale za Hilla zilizo hakikiwa: Kituo cha turathi za Hilla kimetoa kitabu cha (Kashfu Almakhfiyyu min-manaaqibi Almahadiyyu)

Maoni katika picha
Miongoni mwa mfululizo wa nakala kale za Hilla zilizo hakikiwa, kazi inayo fanywa na kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, hivi karibuni wametoa kitabu cha (Kashfu Almakhfiyyu min-manaaqibi Almahadiyyu) cha Haafidh Ibun Batwiriqi Alhilliy aliye fariki kwaka wa (600h).

Kitabu hiki kilikua miongoni mwa vitabu vilivyo potea, kimepatikana kutokana na kazi kubwa iliyo fanywa na Mhakiki Sayyid Muhammad Ridhwa Husseini Aljalaliy, amekusanya kutoka sehemu mbalimbali hadi kupata kitabu kinacho fanana zaidi na kilicho potea, kituo kilifanya kazi ya kusoma na kukagua rejea na faharasi pamoja na kukichapisha katika muonekano mzuri unao endana na hadhi yake.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa umuhimu mkubwa sana katika kazi za uhakiki wa vitabu na nakala kale, na kuvichapisha kupitia taasisi zake maalumu, hadi sasa wamesha chapisha mamia ya vitabu vilivyo fanyiwa uhakiki na sasa vimekua marejeo ya watafiti na wasomi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: