Kikao kimeongozwa na Dokta Swabahu Abu Janaah, katika kikao hiki imesomwa mihtasari ya tafiti tisa, yafuatayo ni majina ya watafiti na zafiti zao:
- 1- Dokta Saidi Jaasim Zubaidiy: (Msimamo wa Shekh Muhammad Jawaad Aljazaairiy katika kurahisisha nahau).
- 2- Dokta Aamali Hussein Alwaan: (Wataalamu wa historia ya mashairi katika hauza ya Najafu karne ya kumi na mbili na kumi na tatu hijiriyya).
- 3- Dokta Qusway Samiri Issa Alhilliy: (Selebasi ya lugha kwa wanachuoni wa hauza – Sayyid Ali bun Twauus kama mfano).
- 4- Dokta Saamir Abdulkaadhim Jalabi: (Historia ya fani za kiarabu – Munjizu Mahmudu Bustaniy kama mfano).
- 5- Dokta Muhammad Abdurahmaan Arifi/ kutoka Misri: (Athari ya Najafu katika kulinda lugha ya kiarabu kwa kusaidia wanachuoni na maktaba kwa ujumla).
- 6- Shekh Imaad Kaadhwimiy / kutoka Atabatu Kadhimiyya tukufu: (Sayyid Hibatu-dini Shaharistani na mchango wake katika lugha ya kiarabu – kuonyesha usomaji kwa ufupi).
- 7- Dokta Aatwiy Abayati / kutoka Iran: (Sifa na utenzi wa mashairi ya Najafu).
- 8- Dokta Ali Khadwiri Haji: (Maandishi ya fani za watu wa Najafu yaliyopo katika hauza ya Najafu).
- 9- Muhammad Munaadhil Abbasi: (Msamiati wa Nahau kwa ibun Ataaiqiy).