Kuhitimisha kongamano na maonyesho ya ubunifu ya pili chini ya msisitizo wa kufanyia kazi matokeo yake.

Maoni katika picha
Alasiri ya Ijumaa (14 Rajabu 1440h) sawa na (22 Machi 2019m) kimefanyika kikao cha kufunga kongamano la wabunifu la pili lililofanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Karbala ni kitovu cha elimu na wanachuoni) lililo endeshwa na muungano wa wabunifu wa kiiraq chini ya ufadhili wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa muda wa siku tatu.

Hafla ya ufungazi imefanyiwa ndani ya jengo la Shekh Kuleini (q.s) ambalo lopo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kuhudhuriwa na watu wengi, ikiwa ni pamoja na wasomo wa sekula na dini na watafiti wa kiiraq, pamoja na jopo la viongozi wa Atabatu Abbasiyya likiongozwa na kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) na katibu wake mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar (d.t), hafla ilifunguliwa kwa kusoma Quráni tukufu pamoja na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ukaibwa wimbo wa taifa na wimbo wa Ataba tukufu.

Halafu Dokta Abbasi Didah ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya uongozi wa Ataba tukufu akaongea, akasema kua: Hakika ubunifu na akili vi vitu vinaenda pamoja, akatoa wito wa kuangalia sheria zilizopo kama zinaendana na mahitaji ya wabunifu wa kiiraq, ni lazima kuwe na aina ya kuwasaidia wabunifu kifedha.

Baada yake ukafuata ujumbe wa kamati ya elimu iliyo simamia kongamano na maonyesho, ulio elezea ujumbe wa mwisho na maazimio, uliwasilishwa na Dokta Khalidi Ajamiy, miongoni mwa aliyo sema ni: “Katika maonyesho haya tulipokea karibu aina (380) za ubunifu, katika hizo tukachagua aina (85), aina zilizo chaguliwa zinawakilisha wabunifu wa Iraq na zinaweza kufanyiwa kazi, na zinaendana na mazingira ya Iraq”.

Kisha Dokta Khalidi Ajamiy akasoma maazimio ya kongamano na maonyesho. Halafu wakatangazwa waliopata alama za juu katika maonyesho na kila mmoja kutokana na aina ya ubunifu wake, kila aina ya ubunifu wametangazwa washindi watatu, aina za utafiti zilikua ni: (Tiba – elimu ya afya – uhandisi – kilimo – elimu ya vitendo) wamepewa midani ya dhahabu, fedha na silva.

Mwisho kabisa wabunifu walioshiriki katika maonyesho ya ubunifu wakapewa zawadi pamoja na kamati iliyo simamia kongamano na maonyesho haya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: