Maoni katika picha
Safari hiyo ipo chini ya usimamizi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, tumeongea na kiongozi wao amesema kua: “Safari hii imeratibiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), yeye ndiye alishauri kuandaa msafara wa kwenda kufanya ziara katika malalo ya bibi Zainabu (a.s) katika kumbukumbu ya kifo chake, safari hii inajumuisha familia za mashahidi walio jitoleo roho zao kwa ajili ya taifa letu tukufu, pamoja na kundi la majeruhi walio umia katika vita ya heshima na utukufu, kutokana na kuitikia kwao wito wa Marjaa uliohami taifa na maeneo matakatifu”.
Wageni wa Hauraa Zainabu (a.s) wameshindwa kuelezea hisia zao walipokua wanahuisha utiifu wao na kuhudumia mazuwaru watukufu, wameshukuru sana jambo hili tukufu walilo fanyiwa na Atabatu Abbasiyya.