Mawakibu za waombolezaji zamiminika katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kuja kuwapa pole kwa kifo cha dada yao na makumi ya mawakibu zingine zinatoa huduma.

Maoni katika picha
Kama kawaida katika siku ya huzuni kwa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), siku ya kumbukumbu ya kifo cha Aqiilah bani Hashim bibi Zainabu (a.s), katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) zinamiminika mawakibu za waombolezaji wa dada yao mtakasifu.

Rair wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riyadh Ni’mah Salmaan ameongea na mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika uingiaji wa mawakibu za kuomboleza katika kumbukumbu za vifo vya Maimamu huanza mapema katika kila tukio, likiwemo tukio la kifo cha bibi Zainabu (a.s), haya ni mazowea ya tangu zamani, watumishi wa kitengo chetu huratibu matembezi ya mawakibu, katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) zinaingilia mlango wa Kibla na baada ya kufanya maombolezo yao huelekea katika malalo ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), wakipitia katika uwanja mtukufu wa katikati ya malalo mawili huku wakiwa pamoja na kundi kubwa la mazuwaru”.

Akabainisha kua: “Idadi ya mawakibu zilizo sajiliwa ndani ya siku mbili imefika (54), maukibu (30) za kuomboleza (matam na zanjiil), na maukibu (24) za kuomboleza na kutoa huduma, maukibu hizo zilikamilisha mapema vibali vyote vya kufanya shughuli zao hapa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: