Kukamilisha walicho anza: Atabatu Abbasiyya tukufu yaikabidhi Atabatu Zainab (a.s) vifaa mbalimbali vya umeme.

Maoni katika picha
Ukarimu wa Abulfadhil Abbasi (a.s) uko wazi, vipi anapokua anatoa kuipa malalo ya dada yake ambaye hakuacha kumuhudumia hadi baada ya kifo chake, jambo hili ni tukufu sana kwa watumishi wake wakiongozwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya aliye sisitiza kusaidia mahitaji yote ya haram takatifu ya bibi Zainabu (a.s).

Na kukamilisha juhudi zilizo anzishwa katika safari zilizo tangulia, hakika msafara wa Ataba tukufu mara hii umebeba vitu kwa ajili ya haram tukufu na mazuwaru watakatifu, miongoni mwa vitu hivyo ni vifaa mbalimbali vya umeme, tumeongea na kiongozi wa idara ya umeme katika kitengo cha usimamizi wa kihandisi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Ali Abdulhussein amesema kua: Ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu umekuja na vifaa tofauti vya umeme, ambavyo vimekabidhiwa kwa awamu mbili, vifaa hivyo ni:

  • 1- Projekta 140 za Radi wart 240.
  • 2- Projekta za kutia joto zitakazo elekezwa upande wa minara miwili ya haram tukufu, kila mnara zitawekwa mbili.
  • 3- Taa (500) zenye uwezo wa kuangazia mita (70) kila moja.
  • 4- Bango la mwanga mkubwa lenye maandishi yasemayo (Amani iwe juu yako ewe jabali wa subira) lenye urefu wa mita (5) na unene wa sentimita (80).
  • 5- Taa maalumu kwa ajli ya ndani ya haram za (Lad 4) zipatazo (140).
  • 6- Kifaa cha UPS kwa ajili ya ndani ya haram chenye ukubwa wa (10 KVA).
  • 7- Taa nyeupe za mapambo zapatayo (600) pamoja na taa (300) za mapambo ya rangi nyekundi na kijani.

Akabainisha kua: Tumekuja na jopo la mafundi watakao fanya kazi ya kufunga taa na mitambo tuliyokuja nayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: