Jopo la mafundi kutoka Atabatu Abbasiyya wanafanya ukarabati katika malalo ya bibi Zainabu (a.s).

Maoni katika picha
Jopo la mafundi kutoka Atabatu Abbasiyya wameanza kazi ya kutendeneza baadhi ya maeneo katika malalo ya bibi Zainabu (a.s) kwenye mji mkuu wa Sirya Damaskas, huu ni muendelezo wa kazi walizo kua wamesha anza kuzifanya siku za nyuma kwa lengo la kulikarabati upya jengo hili tukufu, kwa namna ambayo litawafurahisha watu wanaokuja kulitembelea na kuwawezesha kufanya ziara na ibada kwa Amani na utulivu.

Miongoni mwa kazi zinazo fanywa na jopo hilo la mafundi kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara ya umeme kutoka kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Ali Abdulhussein, ni: “Kufunga taa katika eneo lenye urefu wa mita (100), na upana wa mita (200) na kuziunganisha na mfumo mkuu wa umeme, kwa ajili ya kuzisimamia na kubadilisha rangi zake, taa zenye wat 9, kwa namna ambayo zitaendana na kila tukio kama ilivyo katika Ataba zingine, pamoja na kuweka taa za akiba (200) ambazo ziko tayali kuchukua nafasi ya taa yeyote itakayo haribika, tumefanya pia matengenezo kwa ujumla katika mitambo ya umeme tulio funga siku za nyuma, ikiwemo ile iliyopo ndani ya minara, pamoja na kazi hizo tumeanza kutengeneza na kubadilisha mfumo wa taa katika ukumbi wa wanaume na kwenye ukumbi wa wanawake, sambamba na kutengeneza winchi ya haram tukufu na kuirudisha kazini upya.

Akamaliza kwa kusema: Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya unaojumuisha watumishi wa vitengo viwili, kitengo cha usimamiza ha haram na mambo ya elimu na utamaduni pamoja na kitengo cha usimamizi wa kihandisi, tunatarajia kumaliza kazi kwa wakati katika kumtumikia Aqiilah Zainabu (a.s) na mazuwaru wake watukufu.

Kumbuka kua hizi sio kazi za kwanza, kuna kazi zingine zilizo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya mafundi walio bobea, wakazimaliza kwa namna bora kabisa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: