Atabatu Abbasiyya tukufu yaizawadia malalo ya Hauraa Zainabu (a.s) vifaa vipya vya mawasiliano.

Maoni katika picha
Haram ya Zainabiyya ilikua na haja kubwa ya vitu tofauti, ili kuifanya iwe katika mazingira bora ya kupokea mazuwaru katika matukio yote ya kidini, mahitaji hayo yamepungua kutokana na juhudi za Atabatu Abbasiyya tukufu na safari inazo fanya mfululizo kwenda katika malalo ya Hauraa (a.s), kupitia mafundi wanao kwenda huko wameweza kuweka upya marumaru na kukarabati malalo hiyo tukufu, na kuziba pengo la upungufu wa vifaa, bado jopo la mafundi kutoka Atabatu Abbasiyya lipo katika malalo ya bibi Zainabu (a.s), linaendelea na kazi ya kukarabati malalo hiyo tukufu, wameikabidhi haram ya Zainabiyya vifaa vya kisasa vya mawasiliano.

Kwa maelezo Zaidi kuhusu vifaa hivyo, mtandao wa Alkafeel umeongea na Ustadh Abdul-Amiir Masudi ambaye amesema kua: “Miongoni mwa mahitaji ya lazima katika haram ya Aqiilah Zainabu (a.s) ni kebo ya taa, tumeleta kebo pamoja na vifaa vyake vyote kutoka Iraq na tumesha panga utaratibu wake wote, jambo hili litasaidia Atabatu Zainabiyya tukufu katika sekta nyingi, ikiwa ni pamoja na kuendesha mfumo wa intanet na kamera pamoja na simu, tumeunganisha na simu (2), sambamba na kufunga Haraak –sanduku maalumu lenye mitambo-, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu, kazi zote zitakamilika katika safari ijayo”.

Akaongeza kua: “Kwa upande mwingine tumewasha mtambo wa vipaza sauti uliofungwa na Atabatu Abbasiyya tukufu siku za nyuma, umetumika katika kupokea maukibu zote zilizo kuja katika kumbukumbu ya kifo cha Hauraa Zainabu (a.s), kutoka mikoa tofauti ya Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunamshukuru Mwenyezi Mungu mtukufu na Maulana Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kupata fursa ya kumtumikia Aqiilah Zainabu (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: