Kutokana na manukato ya malalo ya mtumishi wake tunanukisha malalo yake.

Maoni katika picha
Baada ya safasi iliyodumu kwa zaidi ya siku saba, na kufanikiwa kufanya kazi nyingi, leo watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanamalizia safari yao ya sita katika malalo ya Aqiilah bani Hashim bibi Zainabu (a.s), safari hii inamaliziwa kwa kuosha kaburi takatifu na dirisha la malalo yake (a.s) pamoja na kuweka manukato, tena manukato zile zile ambazo hutumika katika dirisha la kaka yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Safari hii imesadifu kumbukumbu ya kifo cha bibi Zainabu (a.s) na imekuja kukamilisha mambo yaliyo fanywa katika safari zilizo tangulia, katika safari hii tumefanya kazi nyingi zilizo changia marekebisho katika malalo tukufu kuanzia sekta ya umeme hadi vifaa, pamoja na mambo ya mawasiliano na vipaza sauti, pia sio siri kuwa wameshirikiana na waombolezaji wa msiba huu, kwa kufanya majlisi za kuomboleza kwa muda wa siku mbili, na kutoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru watukufu.

Mkuu wa haram ya Zainabiyya Mhandisi Muhsin Harbu amesifu kazi nzuri iliyo fanywa na Atabatu Abbasiyya kwa kusema kua: “Tumezowea kila baada ya muda Fulani kupokea ndugu zetu kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu wanaokuja katika haram ya bibi Zainabu (a.s), wanapo fika hutoa huduma mbalimbali, kila wanapokuja huwa tunafanya mawasiliano na viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kuwaeleza mahitaji ya haram, na wao hutupatia kila kinacho hitajika”.

Akaongeza kua: “Daima mimi huwaambia kua huduma hizi zinatakiwa zifanywe na Atabatu Abbasiyya tukufu zaidi kushinda Ataba zingine, kwa sababu Abulfadhil Abbasi (a.s) ndiye mtumishi mkuu wa dada yake bibi Zainabu (a.s), kwa kweli tunaona huduma yake katika kila safari, wanafanya kazi kubwa ya kukarabati ndani ya haram takatifu”.

Akamaliza kwa kusema: “Shukrani za dhati ziufikie uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na watumishi wake, kwa kudumisha mawasiliano na Atabatu Zainabiyya takatifu, tunamuomba Mwenyezi Mungu awape nguzu zaidi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: