Atabatu Abbasiyya tukufu imewekwa mapambo meusi kutokana na kuomboleza kifo cha Imamu Kaadhim (a.s).

Maoni katika picha
Huzuni na simanzi vimetanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu, korido zake zimewekwa mapambo meusi kwa ajili ya kuomboleza kifo cha Imamu wa Saba, Imamu Mussa bun Jafari Alkaadhim (a.s), kwenye kuta zake kumetungikwa vitabaa vilivyo andikwa maneno yanayo ashiria huzuni, kutokana na huzuni kubwa iliyo patikana kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu kama kawaida yake, imeandaa ratiba kamili ya kuomboleza msiba huu, inayo husisha utowaji wa mihadhara ya Dini ndani ya haram tukufu pamoja na kufanya majlisi maalumu kwa watumishi wake ndani ya ukumbi wa utawala, sanjari na kufanya matembezi ya pamoja kwa watumishi wa Ataba mbili tukufu kwa ajili ya kuomboleza msiba huu.

Hali kadhalika vitengo vyote vya Ataba tukufu vimejiandaa kutoa huduma bora kwa kila atakayekuja Karbala ndani ya siku hizi, miongoni mwa mazuwaru na mawakibu za waombolezaji, wanaokuja kumpa pole bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), katika kuomboleza kifo cha Imamu Kaadhim (a.s).

Fahamu kua wafuasi wa madhehebu ya Ahlulbait (a.s) katika kila pembe ya dunia siku ya (25 Rajabu) huomboleza kifo cha Imamu Mussa Alkaadhim (a.s) aliye uwawa kwa sumu na matwaghuti wa zama zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: