Muhimu: Fuatilia matangazo ya matokeo ya shindano la mashairi yatakayo somwa katika kongamano la Rabiu Shahada.

Maoni katika picha
Katika tangazo lililo tolewa na toghuti ya Rabiu Shahada, kamati ya maandalizi imetangaza kuwa hivi karibuni itatangaza matokeo ya mwisho ya kaswida zilizo faulu kushiriki katika shindano litakalo fanyika kwenye kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada la kumi na tano.

Wamesisitiza kua: “Matokeo yatatangazwa siku ya Jumatano (26 Rajabu 1440h) sawa na (3 Aprili 2019m), na kutoa wito kwa washiriki wafuatilie tangazo hilo kwenye toghuti ya kongamano ambayo itatangaza matokeo hayo, kupitia anuani hii: (https://rabee.alkafeel.net/index.php), pamoja na toghuti maalumu za Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya, ambazo ni: (http://www.imamhussain.org/arabic/) na (https://alkafeel.net/).

Fahamu kua shindano la mashairi lipo katika ratiba ya kongamano la mwaka huu la (kumi na tano), baada ya kupendekezwa katika kongamano la kumi na nne (la mwaka jana).

Katika tangazo lililopita, kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahadi ilitangaza kukamilika mchujo wa kaswida zitakazo shiriki katika shindano, ambapo wamepata washiriki wengi kutoka ndani na nje ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: