Mawakibu za kuomboleza zamiminika katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kama kawaida ya wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kila mwaka huwa wanakuja kuomboleza kifo cha Imamu Mussa bun Jafari Alkaadhim (a.s) kutoka kila sehemu, asubuhi ya Jumanne (25 Rajabu 1440h) sawa na (2 Aprili 2019m) wameanza kumiminika katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kuja kumpa pole kutokana na msiba huu mkubwa.

Rais wa kitengo cha mawakibu Husseiniyya cha Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riyadhi Ni’mah Salmaan ameongea na mtandao wa Alkafeel kua: “Kama kawaida katika kila kumbukumbu ya kifo cha Imamu, mawakibu za Karbala hufanya matembezi ya kuomboleza, matembezi hayo huanzia katika eneo la mlango wa Bagdad na huja hadi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wakipitia katika eneo la uwanja wa haram mbili tukufu na kumalizia katika haram tukufu ya Imamu Hussein”.

Akaongeza kua: “Kuhusu mawakibu za kutoa huduma, tumesajili zaidi ya maukibu (50) na tumezipatia mahitai ya msingi kwa ajili ya kurahisisha utendaji wao, kwa lengo la kuwahudumia mazuwaru wanaokwenda katika mji wa Kadhimiyya kuomboleza kifo cha Imamu Mussa bun Jafari Alkaadhim (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: