Katika Atabatu Abbasiyya tukufu: Kuanza vikao vya mada za kitafiti katika kongamano ya kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada.

Maoni katika picha
Asubuhi ya tarehe (4 Shabani 1440h) sawa na (10 April 2019m) imeanza kutekelezwa ratiba ya siku ya pili ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada awamu ya kumi na tano, kimefanyika kikao cha kwanza cha uwasilishaji wa mada za kitafiti na kuhudhuriwa na viongozi wakuu wa kisheria katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya na makatibu wao wakuu pamoja na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Iraq, katika ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Hafla imefunguliwa kwa Quráni tukufu kisha likafuata tamko la ukaribisho lililo tolewa na muongozaji wa kikao hicho Dokta Alaa Mussawi, akaelezea umuhimu wa kufanywa vikao vya uwasilishaji wa mada za kitafiti na makongamano ya aina hii, kwa sababu yanasaidia kupata fikra mpya na kuinua kiwango cha elimu katika umma wa kiislamu.

Kisha zikaanza kwawasilishwa mihtasari za mada za kitafiti kama ifuatavyo:

  • - Utafiti wa kwanza ulikua wa Shekh Dhiyaau Zainu Dini/ kutoka Iraq, utafiti wake unasema: (Utukufu wa Abulfadhil Abbasi).
  • - Utafiti wa pili ulikua wa Sayyid Muniir Khabbaaz/ kutoka Saudia, utafiti wake unasema: (Fiqhi Islahi.. umbo lake, zana zake na hatua zake).
  • - Utafiti wa tatu ulikua wa Sayyid Hashim Haashimiy/ kutoka Kuwait, utafiti wake unasema: (Fikra kutoka katika upotofu hadi kwenye usahihi).

Kikao kimeshuhudia maoni na michango mbalimbali kutoka kwa wahudhuriaji, pamoja na maswali ambayo watoa mada (watafiti) waliyajibu na kusherehesha pale palipo hitaji kushereheshwa zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: