Kwa kuzaliwa Imamu Sajjaad (a.s) zikafunguka chemchem za elimu na hekima katika ardhi.

Maoni katika picha
Katika siku kama leo mwezi tano Shabani mwaka wa (38h) nyumba ya Utume na wafuasi wao pamoja na wapenzi wao walipata furaha kwa kuzaliwa moja ya miezi iliyo bashiriwa na Mtume (s.a.w.w), dunia ilinawirika kwa kuzaliwa Imamu Sajjaad Zainul-Aabidina (a.s) aliyekua chemchem ya elimu na hekima hapa duniani.

Hakika (a.s) ni mfano bora kwa wanaadamu kwa namna alivyo ipa nyongo dunia na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, aliishi na babu yake kiongozi wa waumini (a.s) miaka miwili, na akaishi na ammi yake Hassan miaka kumi, na baba yake Hussein (a.s) miaka kumi na moja, baada ya kufariki baba yake aliishi miaka thelathini na nne, alifia Madina mwaka wa tisini na tano hijiriyya akiwa na miaka hamsini na saba.

Mama yake mtukufu ni: Shahaznaan (Shaharubanu) mtoto wa Yazdajard mfalme wa mwisho wa Saasaaniyyah, mama huyu mtukufu alikua na hadhi kubwa katika ulimwengu wa wanawake wa kiislamu, alikua mwanamke bora katika zama zake. Imepokewa kua Asmai alihadithia kua, binti wa Yazdajard alikuja kwa Ali bun Abu Twalib (a.s) akiwa katika msafara wa wajakazi mia moja, Imamu Ali (a.s) akasema: Mkirimuni hakika huyu ana neema.

Majina yake ya kuniya (a.s) anaitwa: Abu Hassan, Abu Hussein, Abu Muhammad, Abu Abdillahi, Abu Qassim, Abu Khairataini.

Pia anamajina mengi ya laqabu, miongoni mwa majina hayo ni: Sajjaad, Zainul-Aabidina, Dhu Thaqnaat, Zakiyyu, Amiin…, miongoni mwa laqabu mashuhuzi zaidi ni (Zainul-Aabidina), katika laqabu zake pia ni: Sayyidul Aabidina, kama alivyo itwa na babu yake Mtume (s.a.w.w).

Athari zake kielimu: Wanachuoni wameandika hadithi alizokua anafundisha kila siku ya Ijumaa katika msikiti wa Mtume, na katika kipindi cha Hija pamoja na kwenye vikao alivyo kua anafanya na wanachuoni, hadithi zake zinapambanua maarifa ya kiislamu, alikua akizitumia katika kutafsiri Qur’ani na kusherehesha sunna tukufu pamoja na kufafanua idikadi na sheria za kiislamu, na kutatua mambo yanayo tatiza watu, sambamba na mafundisho mengi yaliyo pokewa kutoka kwake, kwa hakika watu wenye akili na wachamungu walipata kile walichokua wamepoteza katika mimbari yake na vikao vyake, miongoni mwa athari zake ni Sahifatu Sajjaadiyya na Risalatul Huquuq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: