Kituo cha upigaji picha nakala kale na faharasi chafanya warsha kuhusu nakala kale katika chuo kikuu cha Mustanswiriyya.

Maoni katika picha
Kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Atabatu Abbasiyya tukufu na chuo kikuu cha Mustanswiriyya katika sekta tofauti ikiwa ni pamoja na kufanya warsha za aina hii, kituo cha upigaji picha wa nakala kale na faharasi chini ya Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya kimeratibu warsha hii kuhusu: (Nakala kale na vielelezo.. malengo yake, uandaaji wake, vifaa vyake na njia za utunzwaji wake), chini ya kauli mbiu isemayo: (undani wa yaliyo pita kwa ujuzi wa kisasa), katika kitengo cha maktaba na taaluma chini ya kitivo cha adabu katika chuo kikuu hicho.

Warsha hiyo imehudhuriwa na idadi kubwa ya wanafunzi pamoja na wakufunzi wao, kituo kimepata fursa ya kujitambulisha pamoja na kuelezea vitengo vyake na majukumu yao, kisha kikaanza kufafanua kuhusu nakala kale, vielelezo, malengo, uandaaji, vifaa na njia za utunzwaji wake, sambamba na kuelezea kazi zinazo fanywa na kitengo cha upigaji picha.

Mwishoni mwa warsha wakufunzi na wanafunzi walioshiriki katika warsha walionyesha kufurahishwa na warsha, hasa katika sekta ya utunzaji wa turathi na nakala kale pamoja na upigaji wa picha na faharasi, wakaipongeza Atabatu Abbasiyya tukufu hasa vituo vyake vya kiutamaduni na kielimu, halafu watumishi wakapewa zawadi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: