Kutokana na mchango wake: Serikali ya Waasit yakishukuri kikosi cha Abbasi (a.s) kwa msaada wake.

Maoni katika picha
Baada ya juhudi kubwa na za wazi zilizo fanywa na kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s), na mchango wake katika kuzuwia hatari za mafuriko na kurudisha hali ya utulivu na amani pamoja na kuondoa maji ya mafuriko yaliyo ukumba mkoa wa Waasit hivi karibuni, kutokana na kuthamini mchango wao, serikali ya mkoa wa Waasit imetoa shukrani nyingi kwa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji.

Msemaji wa kikosi amesema kua muwakilishi wao katika mkoa wa Waasit amepokea barua rasmi kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa Dokta Muhammad Jamili Almayahi ya kuwasifu na kuwashukufu, na kuthibitisha kua mahitaji ya vifaa vya kihandisi vilivyo tumwa na kikosi cha Abbasi yameisha, baada ya kumaliza hatari ya mafuriko katika mkoa wa Waasit kwa mujibu wa barua hiyo.

Kumbuka kua kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kilituma jopo la wahandisi katika mkoa wa Waasit na kikatumia askari wake wa hakiba waliopo katika mkoa huo, kwenda kusaidia serikali kupambana na mafuriko na kuwalinda raia na mji huo kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: