Inatokea hivi sasa: Chini ya utaratibu kamili wa Ataba mbili tukufu na eneo la katikati haram mbili limefurika watu.

Maoni katika picha
Ulipo fika usiku wa mwezi kumi na tano Shabani, watu wamefurika katika haram tukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbadi (a.s) kutoka kila sehemu ya dunia, katika mazingira mazuri ya kiroho huku wakijikurubisha kwa muumba wao wakitokwa machozi na nyoyo zenye unyenyekevu, wakimuomba msamaha, rehma na kukubaliwa ibada zao kwa utukufu wa usiku huu adhim.

Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na uwanja wa katikati ya haram mbili baada ya adhuhuri ya leo watu walianza kumiminika kwa wingi kuja kufanya ziara ya Shaabaniyya, ambayo kilele chake ni karibu na muda wa Isha-aini huku ulinzi ukiwa umeimarishwa pamoja na utowaji wa huduma chini ya watumishi wa Ataba mbili tukufu na kitengo cha katikati ya haram mbili, wote kwa pamoja wamejipanga kutoa huduma bora zaidi inayo endana na ongezeko la idadi ya mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: