Mamia ya sahani za chakula zimetolewa na mgahawa wa Atabatu Abbasiyya kwa mazuwaru.

Maoni katika picha
Mgahawa (mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi ni mwendelezo wa ukarimu wake katika kuhudumia mazuwaru wa Karbala, waliokuja kufanya ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani na kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu wa Zama (a.f), umegawa mamia ya sahani za chakula kila siku kupitia madirisha ya nje, ukiwa ni mwendelezo wa kazi waliyo anza tangu mwanzoni mwa mwezi huu.

Kutokana na msongamano mkubwa wa mazuwaru, mgahawa uliamua kufungua madirisha ya nje kwa ajili ya kugawa chakula, yaliyopo upande wa barabara ya Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na eneo la upande wa mgahawa kwa nje, na kugawa chakula, vinyaji na matunda, kila zaairu alichukua chakula anacho penda.

Kama kawaida katika ziara zinazo hudhuriwa na watu wengi, mgahawa huwapanga mazuwaru katika mistari miwili, wa wanaume na wanawake kwa ajili ya urahisi wa kuwagawia chakula, hii ni kutokana na uzowefu wa miaka mingu katika shughuli ya kugawa chakula, kitengo cha mgahawa wa mwezi wa bani Hashim (a.s) ni mashuhuri kwa kuhudumia mazuwaru, wala sio katika mji wa Karbala peke yake bali kila sehemu ya mazaru huenda kutoa huduma kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: