Arshu Tilawah inaendelea na mahafali zake za kila wiki, imewaalika wasomaji kutoka muungano wa wasoma Quráni tukufu katika mkoa wa Misaan.

Maoni katika picha
Kuna miradi mingi ya Quráni tukufu inayo fanywa na Maahadi ya Quráni ya Atabatu Abbasiyya, miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa Arshu Tilawah, nao unalenga kunufaika na vipaji vya usomaji wa Quráni vya wairaq na kuvionyesha katika ulimwengu wa kiislamu, pamoja na kuviendeleza kwa kufuata utaratibu maalum chini ya walimu walio bobea katika fani za Quráni.

Miongoni mwa mambo muhimu katika mradi huu ni kufanya hafla za usomaji wa Quráni kila wiki ndani ya haram ya Abulfadhl Abbasi (a.s), katika hafla hizo husoma idadi kadhaa wa wadau wa mradi huu, wiki hii wamealikwa wasomaji kutoka muungano wa wasomaji wa Qur,ani wa mkoa wa Misaan.

Wameburudisha masikio ya wahudhuriaji na mazuwaru wa malalo takatifu kupitia wasomaji tofauti, miongoni mwa waliosoma ni Ali Saaidiy msomaji wa Atabatu Abbasiyya, Mauhubina Ahmadi Raadhi Saalim, Ali Muhammad mwanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa na Abdulkhaaliq Asádi Ahmadi mwanafunzi wa semina zinazo endeswa na kituo.

Mazuwaru walijaa pembezoni mwa wasomaji hao wakitafakari aya za Quráni tukufu, zilizo kua zikisomwa kwa sauti murua ndani ya eneo hilo takatifu, huku wengine wakifuatilia mubashara (moja kwa moja) kupitia luninga ya Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: