Kwa picha: Tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu lawa tulizo la macho ya wasomi na wageni wa kongamano la utamaduni wa amani.

Maoni katika picha
Tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu linalo shiriki katika kongamano la utamaduni wa amani la mwaka wa kumi, linalo simamiwa na taasisi ya Imamu Swadiq (a.s) katika mji wa Diwaniyya, kwa kushirikiana na Ataba tukufu, limepata mwitikio mkubwa kutoka kwa wadau wa maonyesho, ambayo ni sehemu ya kongamano hilo, limekua kivutio kikubwa kwao kutokana na aina ya vitabu wanavyo onyesha vinakidhi mahitaji yao ya kifikra na kitamaduni.

Miongoni mwa watafiti wakubwa walio tembelea tawi hilo ni Mheshimiwa Shekh Muhammad Kanáan kutoka Lebanon na Sayyid Muniir Khabbaaz kutoka Saudia na Shekh Hussein Aali Yaasiin mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika mji wa Bagdad, pamoja na wageni wengine wa kongamano kutoka nje ya Iraq, bila kuwasahau viongozi wa kidini, kijamii na wasomi mbali mbali kutoka ndani na nje ya mji wa Diwaniyya, pamoja na wale waliosafiri kwa ajili ya kuja kutembelea maonyesho haya, kwao hii ni fursa muhimu ya kujenga uhusiano na mawasiliano pamoja na kujua aina za vitabu vilivyopo, wameomba kurudiwa tena jambo hili siku zijazo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: