Shekh Kamali Karbalai: Tunapitia changamoto ambazo tunalazimika kupambana nazo kwa kuonyesha malezi mema kimaadili, kijamii, kielimu na kibinaadamu.

Maoni katika picha
Shekh Kamali Karbalai kutoka kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, katika khutuba aliyo toa kwenye hafla ya ufunguzi wa mashindano ya kijana wa Alkafeel ya mwaka wa tatu kwa wanafunzi wa sekondari katika mkoa wa Muthanna amesema kua: “Hakika tunapita katika zama zenye changamoto nyingi, hakuna njia ispokua ni kupambana nazo, tunatakiwa kuonyesha malezi mema, na kujifunza katika madrasa ya Ahlulbait (a.s) ili tuwe mfano mwema kwa kila mtu”.

Akasema pia: “Mwenyezi Mungu anasema ndani ya kitabu chake kitukufu: (Na, Sema. Fanyeni kazi Mwenyezi Mungu ataona kazi yenu na Mtume na waumini), enyi ndugu zangu wapenzi, sisi tupo katika mji mtukufu tunaona mazuri yake, shukrani ziwaendee wazazi wetu na walezi wetu kwa kazi kubwa waliyo fanya ya kudumisha maadili ya ubinaadamu, hakika tunahaki ya kujivunia juhudi zao, pamoja na kujitolea mashahidi, kila kitu Mwenyezi Mungu anaona na Mtume wake na watu wa nyumbani kwake (a.s).

Akaongeza kua: “Mwenyezi Mungu mtukufu anaona kila tunacho fanya, namna gani tunalinda mafanikio haya matukufu tunayo jifaharishia, ikiwa ni pamoja na mashahidi waliotoka katika mji huu kwa ajili ya kuikomboa Iraq, tunalinda vipi damu iliyo mwagika kwa ajili ya taifa hili na misingi ya Dini tukufu iliyo fundishwa na Mtume (s.a.w.w)”.

Akasema: “Hakika Atabatu Abbasiyya tukufu inajitahidi kuibua na kulea vipaji vya vijana kwa ajili ya mustakbali wa umma, nao ni matunda ya kazi nzuri iliyo fanywa na walezi, katika kuifanyia kazi hadithi isemayo (Kila mtu ni mchunga na ataulizwa alicho kichunga), Atabatu Abbasiyya tukufu imekua mstari wa mbele katika kila kitu, kwa ajili ya kuleta maendeleo ya mwanaadamu katika sekta tofauti”.

Shekh Karbalai akasema: “Nyie mmefanya vya kutosha, na sisi katika mji huu mtukufu kupitia vijana wetu na mashahidi wetu, na kwa upevu huu wa fikra tutakua tayali kupambana na changamoto na kulinda misingi hii mitukufu, ili tuweze kufika katika kiwango cha kumnusuru Imamu wa zama (a.f) na tuwe katika hali inayo takiwa katika ulimwengu wa leo”.

Akasema: “Hakika mashahidi walio tolewa na mkoa huu, sawa na mikoa mingine ni dalili ya malezi mema waliyo pata na kuwafanya kuwa fahari ya walimwengu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: