Kumbukumbu ya kukombolewa kwa mji wa Bashiri.

Maoni katika picha
Chini ya anuani isemayo: (Bashiri ni kilele cha utekelezaji na rehma kwa waaminifu) kwa usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji Alasiri ya Jumatano (25 Shabani 1440h) sawa na (1 Mei 2019m) kimefanya hafla kubwa katika mji wa Bashiri, kuadhimisha mwaka wa tatu tangu kukombolewa kwa mji huo kutoka katika makucha ya magaidi wa Daesh, ukombozi huo uliongozwa na kikosi cha Abbasi kwa kushirikiana na vikosi vingine vya wapiganaji, maadhimisho yamehudhuriwa na wageni wengi pamoja na viongozi kutoka mikoa tofauti, pamoja na wawakilishi wa Ataba tukufu na wanajeshi wa serikali na Hashdi Shaábi.

Hafla ilifunguliwa kwa Quráni tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukaimbwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya (Lahnul-Ibaa), ikafuata khutuba ya ukaribisho kutoka kwa watu wa Bashiri iliyo wasilishwa na Mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika mji wa Karkuuk Mheshimiwa Sayyid Qambar Mussawiy, miongoni mwa aliyo sema ni: “Katika siku kama ya leo yalirudi matumaini ya maisha kwa wakazi wa Bashiri, nuru ya taifa letu kipenzi la Iraq ikangáa, katika siku kama ya leo raia watukufu wa Iraq walipata ushindi mkubwa, walithibitisha kua taifa linamajemedari wanao weza kusimama kama ngome imara dhidi ya tishio lolote, wako tayali kujitolea chochote kwa ajili ya taifa lao…”.

Ukafuata ujumbe wa mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji Shekh Maitham Zaidi, akasema kua: “Hakika vita ya kukomboa mji wa Bashiri ilitoa picha ya uzalendo wa kweli na undugu, raia wote wa Iraq walishiriki, vilishiriki vikosi vya Waarabu, Waturkuman na Beshamerka pia walishiriki katika hatua za mwisho kwenye kukomboa mji huo, ndani ya siku moja alishiriki kamanda mwarabu kutoka Kuut na kamanda mturkuman kutoka Taza na kamanda wa kikurdi kutoka Suleimaniyya…”.

Halafu ukafuata ujumbe wa kamanda wa kikosi cha 16 cha Hashdi Shaábi Nabili Bashiri, akasisitiza kua: “Hakika damu takatifu ya wananchi wa Iraq imechanganyika katika ardhi ya Bashiri, hadi ardhi hii imekua takatifu kwa sababu ya damu za mashahidi…”.

Kongamano lilipambwa na kaswida mbalimbali zilizo eleza ushujaa na ujasiri wa wapiganaji waliomwaga damu zao takasifu katika ardhi ya Iraq, kisha wahudhuriaji wakaenda kuangalia maonyesho maalum ya ngawira walizo pata kikosi cha Abbasi (a.s) kwenye vita waliyo pigana katika mji wa Bashiri na maeneo mengine dhidi ya Daesh.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: