Kumiminika mazuwaru katika mji mtukufu wa Karbala Alkhamisi ya kwanza ya mwezi wa Ramadhani.

Maoni katika picha
Watu walianza mapema kumiminika katika mji wa Karbala siku ya Alkhamisi (3 Ramadhani 1440h) sawa na (9 Mei 2019m), kwa ajili ya kufanya ibada za Ijumaa ya kwanza ya mwezi wa Ramadhani katika Ataba tukufu za Karbala.

Mazuwaru walianza kumiminika katika eneo linalo zunguka Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kutoka kila sehemu, wakiwa wanatembea kwa utulivu, tunatarajia kuongezeka idadi ya mazuwaru katika saa zijazo, hufikia kilele chao wakati wa Magharibain na baada yake, huja kufanya ibada maalum za usiku huu jirani na malalo ya Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na huanza kuondoka kidogo kidogo katikati ya usiku hadi baada ya swala ya Alfajri.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu ilikua imesha tangaza kua imekamilisha maandalizi ya kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani, ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu maalum wa kuwahudumia mazuwaru wanaokuja kufanya ibada katika mwezi huu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: