Kwa ushiriki wa wanafunzi (192): Idara ya maelekezo ya Dini kwa wanawake yahitimisha mafunzo kwa wanafunzi wa bweni.

Maoni katika picha
Baada ya miezi miwili ya kufanyika kwa mijadala darasa chini ya ratiba iliyo andaliwa na idara ya maelekezo ya Dini kwa wanawake chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, idara hiyo imehitimisha ratiba hiyo ambayo wameshiriki wanafunzi (192) wa bweni katika chuo kikuu cha Karbala.

Wanafunzi walioshiriki katika program hiyo wameisifu na kushukuru baada ya kukaribishwa katika Atabatu Abbasiyya na kufanya hafla ya kuhitimu kwao, hafla ilikua na vipengele vingi, miongoni mwa vipengele vyake ni mada zilizo tolewa na wanafunzi walio shiriki kwenye program hiyo, wamebainisha kua program hiyo inalenga kuongeza elimu kwa wanafunzi na hilo ndio jambo kubwa kwao, na wametoa wito wa kunufaika na program hiyo na kuifanyia kazi katika maisha ya nyumbani na shuleni.

Pia kuna maswali mengi waliyo ulizwa wanafunzi na wao wakatoa majibu sahihi, walipata nafasi ya kutembelea sehemu mbalimbali za Atabatu Abbasiyya tukufu baada ya kufanya ziara, wakatembelea pia vitalu vya Alkafeel.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: