Kamati ya maandalizi ya kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda awamu ya nne yatangaza shindano la makala bora na yatoa wito wa kushiriki.

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la fatwa ya kujilinda awamu ya nne inatoa wito kwa waandishi wa habari na wadao wa habari na utamaduni, washiriki katika shindano la makala bora kuhusu fatwa tukufu ya kujilinda na ushujaa wa Hashdi Sha’abi.

Shindano lipo katika ratiba ya kongamano litakalo simamiwa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ikiwa ni kuadhimisha kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda chini ya kauli mbiu isemayo: (Nyie ni fahari yetu na utukufu wetu tunajivunia nyie katika umma zote).

Kamati imeweka vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili, nayo ni kama yafuatavyo:

 • 1- Mshiriki anahaki ya kuchagua aina ya uandishi atakao ona unafaa, (makala maoni, makala tunzi au makala elezi) maudhui yake ihusiane na fatwa tukufu ya kujilinda au Hashdi Sha’abi.
 • 2- Makala ielezee ushujaa wa Hashdi Sha’abi kwa ujumla (sio kwa umahususi) namna walivyo linda taifa na kutekeleza misingi ya kibinaadamu pamoja na kulinda mazingira.
 • 3- Makala iandikwe kwa lugha faswaha ya kuirabu na itimize masharti ya makala: -muonekano mzuri, lugha sahihi, uwiyano wa maneno na ufupisho-.
 • 4- Isiwe iliwahi kusambazwa kabla, na iandikwe na mshiriki mwenyewe, asikopi au kuandikiwa na mtu mwingine.
 • 5- Maneno yake yasiwe chini ya (300) na yasizidi (700).
 • 6- Isiwe na maneno ya dharau au matusi au mambo yanayo onyesha utovu wa adabu.
 • 7- Hairuhusiwi kuandika zaidi ya makala moja.
 • 8- Kamati ya maandalizi inahaki ya kuondoa kwenye shindano makala yeyote ambayo haitakamilisha masharti.
 • 9- Mshindi yeyote atakaye bainika kushinda kwa kutumia hila zawadi yake itazuwiliwa.
 • 10- Mshiriki haruhusiwi kuomba makala yake baada ya kuikabidhi kwenye kamati, na makala hiyo itakua haki ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu.
 • 11- Makala ziandikwe kwa kutumia program wa (ward) na iwekwe kwenye (CD) na kukabidhiwa katika kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na wasifu (cv) ya muandishi, au itumwe kwa barua pepe ifuatayo (info@alkafeel.net).
 • 12- Mwisho wa kupokea makala ni (30 Mei 2019m).

Zawadi iliyo pangwa kwa washindi wa tano wa mwanzo ni (100,000) dinari laki moja za Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: