Idara ya ustawi wa jamii katika mkoa wa Diyala: Inatoa futari kwa mazuwaru wa Maimamu wawili Askariyain (a.s) na kugawa vikapu vya chakula kwa familia za mashahidi na masikini.

Maoni katika picha
Idara ya ustawi wa jamii katika mkoa wa Diyala ni sawa na idara zingine za Atabatu Abbasiyya tukufu, zinapambana kutafuta fadhila za mwezi mtukufu wa Ramadhani, inawaandalia futari mazuwaru wa Maimamu wawili Askariyan (a.s), sambamba na kugawa vikapu vya chakula kwa familia za mashahidi na masikini.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara hiyo Sayyid Hassan Qaswaab, akaongeza kua: “Tangu ulipo ingia mwezi wa Ramadhani tumekua tukitekeleza ratiba tuliyo jipangia kwa baraka za Atabatu Abbasiyya, miongoni mwa ratiba yetu ni kugawa vikapu vya chakula kwa familia za mashahidi na masikini, tunatarajia kufikia idadi kubwa ya familia hizo zenye mahitaji”.

Akaendelea kusema kua: “Idara pia imekua ikiandaa futari kwa ajili ya mazuwaru wa Maimamu wawili Askariyan (a.s), hii sio mara ya kwanza, idara ipo wakati wote katika eneo hili takatifu, ndani ya mwezi huu na katika miezi mingine, lakini mwezi huu tumeongeza uwepo wetu kwa ajili ya kutoa huduma ya futari kwa mazuwaru, tunagawa futari kupitia maukibu iitwayo (Saairuna ila Llah) na maukibu ya watu wa Hawishi pamoja na maukibu ya Sayyid Muhammad na maukibu Mudhifu Imamu Hussein (a.s) iliyopo karibu na haram mbili takatifu”.

Akasisitiza kua: “Tunaendelea na ratiba hii pia kuna vipengele vingine tutavitekeleza siku zijazo hadi siku za Iddi tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: