Dondoo za kumbukumbu za Ramadhani: Mwezi kumi na mbili Ramadhani ni siku ambayo Mtume aliunga undugu baina ya Muhajirina na Answari na baina yake na ndugu yake mtoto wa Ammi yake.

Maoni katika picha
Umma wa kiislamu katika siku ya leo –mwezi kumi na mbili Ramadhani- inakumbuka siku ya kuunga undugu, baina ya Muhajirina na Answari katika mji wa Madina mwaka 1 au 2 Hijiriyya, kazi ya kwanza aliyo fanya Mtume (s.a.w.w) baada ya kujenga msikiti ni kuunga undugu baina ya Muhajirina na Answari, undugu wenye misingi ya kiimani, na kuonyesha hisia za mapenzi, kusaidiana, kulindana, kuliwazana, ukawa undugu wenye mfungamano imara, alipokua Maka kabla ya kuhama (hijra) uliunganisha undugu baina ya Muhajirina, kisha akaunganisha tena undugu baina ya Muhajirina na Answari baada ya kuhamia Madina.

Mtume (s.a.w.w) alimpa ndugu kila Mhamiaji katika watu wa Madina (Answari), kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) akamfuata akiwa macho yake yanalengalenga machozi akasema: (Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, umeunga undugu wa maswahaba wote, mimi haujaniunga undugu na yeyote?) Mtume (s.a.w.w) akasema: (Ewe Ali.. haujaridhika mimi kua ndugu yako?) akasema (a.s): (Nimeridhika ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu) akasema (s.a.w.w): (Wewe ni ndugu yangu duniani na akhera).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: