Ugawaji wa futari kwa jina la mkarim wa Ahlulbait (a.s).

Maoni katika picha
Ni wazi kwa kila mtu kua Maimamu wa Ahlulbait (a.s) ni kilele cha utukufu na ukarimu, kila mmoja kati yao ana sifa maalum, wote ni wakarimu, lakini Imamu Hassan Almujtaba (a.s), sifa yake maalum ni ukarim, anaitwa Mkarim wa Ahlulbait (a.s), naye ni miongoni mwa watu wanne watukufu waliotajwa katika riwaya.

Kutokana na utukufu wake pamoja na ratiba ya kongamano hili la kuadhimisha kuzaliwa kwake linalo simamiwa na kamati ya miradi ya hilla Mji wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kwa kushirikiana na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Hassan Almujtaba –a.s- ni nuru iangazayo na kiongozi wa kufatwa) ratiba ya kugawa futari kwa jina la Imamu Hassan (a.s) imeanza kutekelezwa tangu siku tano zilizo pita, katika Maqaamu ya Radu-Shamsi ya Imamu Ali (a.s) kwenye mkoa wa Baabil.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi Mhandisi Hassan Hilliy ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Ratiba ya kugawa futari ya kutabaruku na tukio hili, ni moja ya shughuli zilizo zoweleka kufanywa na kamati inayo simamia kongamano hili tangu kuanzishwa kwa kongamano, huandaliwa futari kila siku na kuigawa kwa watu wanaokuja kutembelea Maqaam au kwa mtu yeyote anaye taka futari hiyo, hugawa chai, juisi na maji pia baada ya futari”.

Kumbuka kua kongamano hili hufanywa kila mwaka kwa ajili ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s), linalenga kuonyesha nafasi tukufu ya Imamu (a.s) na kubainisha msimamo wake dhidi ya kiongozi wa zama zake ambaye ni Muawiya, pamoja na kuangalia mitihani aliyo pata (a.s) katika uhai wake, na kutaja baadhi za usia na hadithi za Imamu (a.s) kuhusi tabia njema na siri za ibada, sambamba na kuangalia namna ya kufanyia kazi misingi ya malezi na ubinaadamu aliyo fundisha (a.s), ambayo inaendana na mazingira halisi ya jamii tunazo ishi kwa sasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: