Kwa mwitikio na mahudhurio makubwa: Mashindano ya vikundi yahitimisha hatua ya pili.

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mkarimu wa Ahlulbait Imamu Hassan Almujtaba (a.s), hatua ya pili ya mashindano ya turathi ya vikundi yanayo fanyika ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani yamehitimishwa katika majengo ya makazi ya Abbasi, yanayo simamiwa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kikao cha mwisho cha hatua ya pili kimehusisha kikundi cha (Alwitru Mautuur) na (Alwaafi), kimeshinda kikundi cha (Alwitru Mautuur) kwa kupata alama (18-10) na kufanikiwa kuingia hatua inayo fuata, ambapo kutakua na mizunguko mitatu na watakao shinda wataingia nusu fainali.

Hali kadhalika wamefanya hafla ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s), ambayo ilihutubiwa na makamo rais wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kubinaadamu Shekh Ali Asadiy, alimzungumza nafasi ya Imamu Hassan (a.s) katika kufundisha Imani ya kiislamu ya kuvumiliana na elimu ya Ahlulbait (a.s), kwa kutoa mifano ya mambo yaliyo jiri wakati wa uhai wa Imamu (a.s), hafla ilipambwa na kaswida zilizo onyesha mapenzi ya kizazi cha Mtume pamoja na Imamu Hassan (a.s).

Washiriki wamesema kua uhuishaji wa matukio (minasaba) ya Ahlulbait (a.s) unasaidia kujua dhulma walizo fanyiwa Maimamu watakasifu (a.s), na wakasisitiza umuhimu wa kushikamana na Ahlulbait (a.s) na kufuata mwongozo wao mtukufu, na wakaishukuru Atabatu Abbasiyya kupitia kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kwa kuandaa mashindano haya.

Tambua kua mashindano ya turathi ya vikundi yanahusisha maswali ya aina mbalimbali kama ifuatavyo: (viongozi na wanachuoni, shule za dini, serikali, nani msemaji?, vitabu na maktaba, ushairi na washairi, malalo na maqaam, Quráni na maarifa ya Quráni, maswali kwa ujumla) kuna kamati maalum ya kuuliza maswali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: