Kuhitimishwa kwa program za kongamano la kuadhimisha kuzaliwa kwa mkarimu wa Ahlulbait (a.s).

Maoni katika picha
Ukumbi wa Shahidi Ubaidi katika wakfu Shia/ tawi la mkoa wa Baabil jioni ya Jumatano (16 Ramadhani 1440h) sawa na (23 Mei 2019m) umeshuhudia kuhitimishwa kwa kongamano la kumi na mbili la kuadhimisha kuzaliwa kwa mkarimu wa Ahlulbait (a.s), lililo simamiwa na kamati kuu ya miradi ya Hilla mji wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), kwa ufadhili wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Hassan Almujtaba –a.s- ni nuru iangazayo na kiongozi wa kufatwa), katika kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake (a.s).

Hafla ya ufungaji imehudhuriwa na viongozi wa kidini, kiutamaduni na kisekula, na ugeni ulio wakilisha Ataba mbili tukufu pamoja na watu wengi miongoni mwa wakazi wa mji huu, ilifunguliwa kwa Quráni tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu zikafuata khutuba kutoka kwa wanafunzi ambao ni Muhammad Hussein na Ali Saáduun, ambao ni washindi wa shindano la kuhifadhi khutuba ya Imamu Hassan (a.s), mradi ambao walishiriki wanafunzi (220) kutoka shule (116).

Baada ya hapo akapanda jukwaani mtafiti wa hauza Shekh Ali Ghazwi na kuwasilisha muhtasari wa utafiti uitwao: (Sharíyya ya Imamu Hassan –a.s- katika mtazamo wa wasiokua Imamiyya.. ibun Kathiir kama mfano) akabainisha kua: “Sharíyya ya ukhalifa wa Imamu Hassan kwa Imamiyya hukuna tatizo loloto, ni amri ya Mwenyezi Mungu wala haiwezekani kupewa fulani na fulani, kuna ushahidi mwingi kuhusu jambo hilo, lakini tumeangalia kitabu cha ibun Athiir kwa kutolea ushahidi kua Imamu Hassan (a.s) ni khalifa wa tano, ametaja hadithi nyingi zinazo thibitisha hilo”.

Ukafuata wakati wa shairi lililosomwa na Mustwafa Ali Swalehe, kisha zikatolewa zawadi kwa viongozi mbalimbali na watu waliochangia kufanikiwa kwa kongamano hili, lililokua na vipengele vingi vinavyo mzungumzia Imamu Hassan (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: