Kukumbuka kifo cha kiongozi wa waumini (a.s): Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya majlisi za kuomboleza.

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba maalum ya kuomboleza kifo cha wasii wa mbora wa Mitume na Manabii Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), zinafanywa majlisi za kuomboleza msiba huu mkubwa kwa umma wa waislamu ulio tokea mwaka wa arubaini Hijiriyya.

Majlisi zinafanywa asubuhi kila siku na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kundi ya mazuwaru wanaokuja kumpa pole mwanae (a.s) na kuhuisha utiifu wao kwake huku wakiwa na huzuni kubwa kwa msiba ulio wapata watu wa nyuma ya Mtume (a.s), uliotokana na jeraha la upanga aliopigwa kichwani na mal-uni Ibun Muljim akiwa kwenye mihrabu Alfajiri ya mwezi kumi na tisa Ramadhani mwaka wa 40 hijiriyya.

Majlisi hizo zinahutumiwa na Sayyid Adnani Mussawi kutoka kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, mihadhara yake itadumu siku zote tatu za kuomboleza, inahusu utukufu wa Imamu Ali (a.s), na namna alivyo jitolea katika kupigania Dini ya Mwenyezi Mungu hadi pumzi yake ya mwisho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: