Kwa picha: Kukamilika kwa hatua ya taono na ya mwisho katika uwekaji marumaru kwenye haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Hivi karibuni imekamilika hatua ya tano ya kuweka marumaru uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kazi iliyo anza zaidi ya miezi minne iliyopita, upande wa kusini kati ya mlango wa Kibla na Imamu Hassan (a.s), kazi ya mradi huu inaelekea mwisho, kulikua na kazi ya maandalizi katika eneo lililopo kati ya mlango wa Imamu Hassan na Swahibu Zamaan (a.f) upande wa magharibi wa haram tukufu.

Haram ilikatwa sehemu tofauti wakati wa kazi ya kuweka marumaru, ili kazi hiyo isizuwie harakati za mazuwaru, baada ya kumaliza ujenzi wa kipande kimoja kilifunguliwa na kuanza kutumika kisha tunaingia kipande kingine, tumefanya hivyo hadi tumemaliza kuweka marumaru katika vipande vyote.

Kazi inaendelea vizuri na inatarajiwa kukamilika ndani ya muda ulio pangwa pamoja na changamoto za utendaji, sambamba na uwekaji wa marumaru pia kuna kazi zingine tunazo fanya, kama utengenezaji wa mifumo inayo pita chini ya marumaru, kama vile mfumo wa umeme na maji taka, na kutoa marumaru za zamani na kusawazisha ardhi, kazi hiyo imefanywa na kitengo cha uangalizi wa kihandisi.

Kumbuka kua mradi wa kuweka marumaru katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ni miongoni mwa miradi inayo kamilisha miradi iliyo tekelezwa awali, umefanywa kutokana na uharibifu mkubwa uliotokea katika marumaru za zamani, ulio haribu muonekano wa haram tukufu kwa sababu ya ukongwe wa marumatu hizo, kwani zilikua na zaidi ya miaka (50), ndipo uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ukaamua kutekeleza mradi huu kwa ajili ya kurudisha muonekano mzuri kwenye bustani miongoni mwa bustani za peponi, kwa namna ambayo inaongeza furaha katika moyo wa zaairu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: