Kutoka Basra hadi Tikrit: Futari ya mwezi wa Ramadhani inayo tolewa na idara ya ustawi wa jamii ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Maoni katika picha
Pamoja na ongezeko la joto na umbali idara ya ustawi wa jamii ya Atabatu Abbasiyya haijaacha kutoa misaada kwa wapiganaji wa serikali na hashdi Shaábi watukufu waliopo maeneo tofauti hapa nchini, hivi karibuni msafara wa idara ya ustawi wa jamii kutoka Basra ulikwenda Tikrit kutoa misaada mbalimbali pamoja na futari kwa wapiganaji waliopo huko.

Msafara huo umetembelea kituo cha Spaika na eneo la Swiniyya, na kugawa futari kwa wapiganaji waliopo katika maeneo hayo, sambamba na kutoa vikapu vya chakula maalum kwa ajili ya mwezi wa Ramadhani kwa wapiganaji hao vitakavyo tumika kwa siku kadhaa.

Wapiganaji waliotembelewa wametoa shukrani nyingi kwa idara ya ustawi wa jamii ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kuendelea kuwakumbuka na kuwasaidia wakati wote, wakasema kua hili sio geni kwa Atabatu Abbasiyya kwani imekua mstari wa mbele kuwasaidia toka siku ya kwanza ilipo tolewa fatwa tukufu ya kujilinda hadi leo.

Fahamu kua idara ya ustawi wa jamii ya Atabatu Abbasiyya inaendelea pia kutoa misaada ya kibinaadamu kwa mayatima na familia za mashahidi na masikini kila sehemu ya Iraq katika kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: