Kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu kinahitimisha majlisi za kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini (a.s).

Maoni katika picha
Kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu chini ya Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya kimehitimisha majlisi za kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini na bwana wa mawasii Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), majlisi hizo zimefanywa kwa muda wa siku tatu (19, 20, 21) katika mwezi wa Ramadhani tukufu.

Majlisi zilifanyika ndani ya uwanja wa eneo la katikati ya haram mbili tukufu, katika majlisi hizo wameshiriki waimbaji kadhaa walio imba kaswida za kuomboleza msiba wa Imamu Ali (a.s), na zilikua zikihudhuriwa na watu wengi.

Kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu kiliandaa sehemu maalum za kufanyia majlisi, pamoja na kutengeneza majukwaa na kuwapanga vizuri mazuwaru walioshiriki katika majlisi hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: