Zaidi ya vikao (26) vya usomaji wa Quráni viko chini ya usimamizi wa tawi la Maahadi ya Quráni katika mkoa wa Najafu Ashrafu.

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu ya Atabatu Abbasiyya imesema kua tawi lake la mkoa wa Najafu ndani ya mwezi wa Ramadhani limesimamia vikao vya usomaji wa Quráni zaidi ya (26) katika maneneo tofauti ndini ya mkoa huo, na vinaendelea hadi mwisho wa mwezi.

Mkuu wa Maahadi Shekh Jawadi Nasrawi akaongeza kua: “Tumezitumia siku za mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kusoma Quráni kwa mazingatio, kwa kiasi cha kumuwezesha mtu kupata uongofu na nuru, ikiwa ni sehemu ya kufanyia kazi maneno ya Imamu Baaqir (a.s) yasemayo: (Kila kitu kina msimu na msimu wa Quráni ni mwezi wa Ramadhani), ndipo tawi la Maahadi katika mkoa wa Najafu likaamua kusimamia vikao vya usomaji wa Quráni katika maeneo tofauti ndani ya mkoa huo.

Akasema: Usomaji wa Quráni ni moja ya harakati inayo fanywa na Maahadi katika mwezi wa Ramadhani, ndani ya misikiti na Husseiniyya, na hushiriki wasomi mahiri pamoja na kundi kubwa la waumini, pia ni sehemu ya utaratibu wa Atabatu Abbasiyya kuhakikisha wanaeneza utamatumi wa kusoma Quráni katika jamii”.

Kumbuka kua Maahadi ya Quráni tukufu hufanya hafla na vikao mbalimbali vya usomaji wa Quráni ndani ya mji mtukufu wa Karbala na mikoa mingine, kwa ajili ya kueneza utamaduni wa kusoma Quráni katika Jamii, na kuandaa kuzazi kinacho fuata muongozo wa Quráni na kizazi kitakasifu, Maahadi inaratiba makhsusu ya mwezi wa Ramadhani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: