Matarajio ya kuandama mwezi wa Shawwal na sikukuu tukufu ya Idul-Fitri.

Maoni katika picha
Mwezi unatarajiwa kuonekana jioni ya Jumanne (29 Ramadhani 1440h) sawa na (4 Juni 2019m), unatarajiwa kuonekana kwa macho wakati wa kuzama jua saa (1:05) jioni katika anga la mji wa Najafu kama kukiwa hakuna mawingu.

Taarifa hiyo ipo katika jeduali la nyakati za mwezi muandamo lililopo katika mtandao wa ofisi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani katika mji wa Najafu, taarifa inasema kua: Mwezi mtukufu wa Shawwal unatarajiwa kuandama jioni ya Jumanne (29 Ramadhani 1440h) sawa na (4 Juni 2019m) katika anga la mji wa Najafu wakati wa kuzama jua saa moja (1) na dakika tano (5) utakua na muinuko wa taraja (11) na dakika (39). Utabakia angani kwa muda wa saa moja (1) na dakika mbili (2), mwezi utakua na ukubwa wa (%1,81), unatarajiwa kuonekana ukiwa mdogo.

Kumbuka kua taarifa hii inatokana na elimu ya nyakati za miezi miangamo sio tangazo rasmi la kuandama kwa mwezi kutoka kwa Marjaa Dini, kwa sababu mwanzo wa mwezi huthibiti baada ya mwezi kuandama kisheria, tunaomba kila mtu kesho aangalie mwezi na atakaye uona atupe taarifa kwa atakaye yeza, tunaomba msitusahau katika dua zenu.

Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: