Vipengele muhimu alivyo ongea Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya Ijumaa

Maoni katika picha
Katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) leo (3 Shabani 1440h) sawa na (7 Juni 2019m) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai Marjaa Dini mkuu amezungumzia vipengele vingi vya kimaadili na kimalezi vinavyo endana na mazingira halisi tunayo ishi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

 • - Katika maisha yote ya Mtume (s.a.w.w) na kuamiliana kwake na watu alikua mwenye huruma, mpole, mtaratibu na mwenye mapenzi na watu.
 • - Upole ni msingi muhimu katika uhusiano wa kijamii na unaweza kusaidia kutekeleza majukumu yenu.
 • - Kila mtu anahitaji kuamiliana na watu hata kama akiwa tajiri kiasi gani.
 • - Maisha ya kijamii na kiuchumi msingi wake ni kusaidiana na kupendana na msingi wake ni kuhurumiana.
 • - Hakuna mtu anaye weza kukamilisha mahitaji yake na kutatua changamoto peke yake lazima atahitai ushirikiano ambao msingi wake ni huruma.
 • - Kutokana na umuhimu wa huruma Mwenyezi Mungu mtukufu ameiweka katika maumbile ya mwanaadamu.
 • - Mtu yeyote asiyekua na huruma hana ubinaabamu, atakua sawa na kiumbe mwingine.
 • - Aya tukufu na hadithi za Mtume zimesisitiza umuhimu wa kupambika na sifa ya huruma.
 • - Kila mtu hadi Manabii na Mitume wanahitaji huruma ya Mwenyezi Mungu, pamoja na kumtii na kumuabudu bado tunahitaji huruma yake.
 • - Lazima tuhurumiane baina yetu maisha hayawezi kua mazuri bila kuhurumiana.
 • - Mwenyezi Mungu mtukufu ameweka huruma katika mfumo wa fikra.
 • - Sio kua huruma inatakiwa wakati wote, kuna baadhi ya wakati na mazingira ukatili unahitajika.
 • - Kwa bahati mbaya huruma imetoweka kwa kiasi kikubwa katika maisha.
 • - Misinqi muhimu ya huruma ni mtu kuihurumia nafsi yake na kuilinda na adhabu za Mwenyezi Mungu pamoja na kuiepusha na shari zake.
 • - Ndani ya kila nafsi kuna mvutano baina ya shari na kheri tunatakiwa kuzuwia nafsi zetu zisidumbukie katika shari na maasi.
 • - Kosa kubwa zaidi kwa mwanaadamu ni kuondoa aibu katika nafsi yake na kufanya ukatili.
 • - Upole unaendana na aibu na humfanya mtu afuate misingi sahihi ya maisha inayo kubalika kiakili.
 • - Kasoro kubwa katika jamii zetu ni kukosekana kwa taasisi za serikali au za kiraia zinazo shughulika na kujenga watu kiroha na kimaadili katika familia na jamii.
 • - Tunatakiwa kutilia umuhimu katika kujenga misingi ya kimaadili na kijamii kama tunavyo tilia umuhimu katika kutafuta dunia.
 • - Tunatakiwa kuingiza tabia ya kuhurumiana katika jamii na kwenye mfumo wa maisha.
 • - Mfumo mzima wa maisha ikiwa ni pamoja na sekta ya siasa unatakiwa kua wa kuhurumiana.
 • - Mtawala yeyote anatakiwa kua na huruma katika moyo wake itakayo msukuma kuhudumia watu na kutatia shida zao.
 • - Mtawala anatakiwa atumie alicho nacho kwa ajili ya kuwahudumia watu na kusaidia wanyengo.
 • - Sifa muhimu kwa mtawala anatakiwa kua mpole na mwenye huruma ili awafanyie watu wote uadilifu.
 • - Mtawala akiwa na huruma atanufaisha watu wengi na uadilifu utaenea kwa wote.
 • - Sifa kubwa ya kiongozi mwenye mafanikio ni yule anayetumia alicho nacho kuhudumia watu.
 • - Baba anatakiwa kua mwenye huruma, upole na mapenzi kwa familia yake na awalinde na mabaya sambamba na kuwatengenezea maisha mazuri.
 • - Huruma inatakiwa kua sifa kuu katika jamii.
 • - Baadhi ya watu wanaroho mbaya hufanya ukatili na kudhulumu haki za watu.
 • - Mwenyezi Mungu mtukufu ameweka msingi wa uhusiano wa wanandoa ni mapenzi na huruma wanatakiwa kuishi hivyo.
 • - Ndugu zangu waumini fanyieni kazi mambo haya.
 • - Utakapo ona ndugu yako anatatizo linatakiwa likuumize kama vile limekupata wewe.
 • - Muone ndugu yako kua ni sehemu yako kama unavyo umia na kiungo kimoja cha mwili wako mwili mzima unakosa raha.
 • - Huruma ndio ikusukume kumfariji na kumsaidia mwenye matatizo.
 • - Usiwe na roho ngumu, unaona mtu anateseka na njaa na ufakiri matatizo yamemsonga kila kona halafu wewe unamcheka na kumpuuza.
 • - Kuhurumiana ni muhimu kwetu sote, tukihurumiana Mwenyezi Mungu atatuhurumia na atateremsa rehema na baraka zake kwetu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: