Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umeshiriki katika ufunguzi wa kongamano la kitamaduni la balozi awamu ya tisa.

Maoni katika picha
Kongamano la kitamaduni la balozi linafanyika kwa mwaka wa tisa mfululizo katika msikiti mtukufu wa kufa, na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya watu na wawakilishi wa Ataba na mazaru tukufu za Iraq pamoja na ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya, kongamano limefunguliwa kwa Quráni tukufu pamoja na surat Fat-ha kwa aili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukasomwa wimbo wa Masjid Kufa na kikosi cha balozi (Safiir).

Ukafuata ujumbe wa katibu mkuu wa Masjid Kufa Sayyid Muhammad Majidi Mussawi, akasema kua: “Ni furaha kubwa kusimama mbele yenu na kuwakaribisha katika mji wa kiongozi wa waumini (a.s), katika kumbukumbu ya ujio wa Muslim bun Aqiil (a.s) katika mji wa Kufa akiwa na barua ya bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s), tunamshukuru kila aliye hudhuria kutoka mikoa tofauti ya Iraq na nchi mbalimbali.

Baada yake ukafuata ujumbe wa kiongozi wa wakfu Shia Sayyid Alaa Mussawi ambaye amesisitiza kufuata mwenendo wa Imamu Ali (a.s), kiongozi wa waumini alipita katika njia ambayo haukupitwa na yeyote, tangu mtihani wa Saqifa alikaa nyumbani kwake kwa ajii ya kulinda misingi ya Dini ya kiislamu.

Kasha ukafuata ujumbe wa Dokta Abdu-Ali kutoka wizara ya malezi na ufundishaji wa kifaransa, aliongea uzowefu wake na akaonyesha picha halisi ya kiongozi wa waumini, pamoja na utafiti aliofanya kuhusu Imamu Ali (a.s) hususa katika kitabu cha Nahjul-Balagha, na kwamba ameandika masomo ya Aqida kutoka ndani ya kitambu hicho.

Akapanda mimbari mshairi wa kimisri Ahmadi Bukhiti, akaimba kaswida kuhusu kuwapenda Ahlulbait (a.s), kisha ikaonyeshwa filamu inayo elezea historia ya kongamano hili namna lilivyo anzishwa na hadi sasa linafanyika kwa mwaka wa tisa.

Hafla ikafungwa kwa kutoa zawadi ya Sayyid Muhammad Ali Halo (r.a) aliye kua katika kamati ya kongamano hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: