Jioni ya Ijumaa (10 Shawwal 1440h) sawa na (14 Juni 2019m) imefanyika nadwa ya kielimu kuhusu ugaidi baada ya Daesh, ulikua mkutano wa amani ambo wageni kutoka Atabatu Abbasiyya wameshiriki, miongoni mwa ratiba ya wiki ya Abulfadhil Abbasi (a.s) awamu ya pili, inayofanywa kwa kushirikiana na jumuwiya za Dini za Ulaya, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na watafiti wa kisekula na vituo tofauti vya utafiti kutoka nchi za Ulaya na za kiarabu na kiislamu.
Nadwa hii ni sehemu ya ratiba ya wiki ya Abulfadhil Abbasi (a.s) awamu ya pili, imefanyika sambamba na kumbukumbu ya mauwaji ya Spaika.
Yamejadiliwa mambo mbalimbali yanayo husu namna ya kumaliza tatizo la ugaidi, na kuweka amani na utulivu katika jamii, pamoja na kuzungumzia changamoto za kijamii, na mchango wa vyombo vya habari katika kutangaza fikra potofu ukiwemo ugaidi, pamoja na kuchambua sheria za kimataifa kwa ujumla, na sharia za Iraq.
Kumbuka kua lengo la nadwa hii ni kutoa huduma za kielimu na kitamaduni na kuifanya kua kiini cha elimu na maarifa.