Juhudi kubwa zinafanywa na idara ya vipaza sauti ya eneo la katikati ya haram mbili tukufu.

Maoni katika picha
Wengi ni wanaeshi wasio julikana wanafanya kazi usiku na mchana, kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri kwa mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) ya kufanya ziara na ibada ndani ya malalo au katika uwanja wa katikati ya haram mbili, miongoni mwa wanajeshi hao ni mafundi wa vipaza sauti wa kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, hivi karibuni wamekarabati na kufunga zaidi ya vipaza sauti (75) katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu na maeneo jirani.

Kiongozi wa idara ya vipaza sauti Ustadh Swabri Abduwanani ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hivi karibuni tumekarabati na kufunga zaidi ya vipaza sauti (75) katika uwanja wa eneo la katikati ya haram mbili na maeneo yanayo zunguka uwanja huo, kazi hiyo ni sehemu ya majukumu yetu”.

Akaongeza kua: “Kama mnavyo jua kila siku huswaliwa swala za jamaa katika uwanja wa katikati ya haram mbili, pamoja na ibada zingine pia hufanywa makongamano na mahafali mbalimbali, bila kusahau matangazo mfululizo yanayo tolewa na idara ya waliopotelewa chini ya kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu, matangazo hayo yanategemea vipaza sauti hivyo, kwa hiyo inatulazimu kua na vipaza sauti vinavyo fanya kazi saa 24”.

Fahamu kua idara ya vipaza sauti hufanya kazi kubwa wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na watu wengi, pamoja na siku za Ijumaa kila wiki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: