Maoni katika picha
Swafaau Adnani mmoja wa watumishi wa idara hiyo amesema kua: “Tunafanya kazi za aina tofauti ikiwemo miradi ya ujenzi pamoja na kutengeneza vitu vinavyo hitajika katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Akaongeza kua: “Watumishi wa idara yetu wanafanya kazi kwa muda mrefu, kwa ajili ya kumtumikia Abulfadhil Abbasi (a.s) na mazuwaru wake”.
Fahamu kua idara ya mafundi chuma chini ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi hufanya kazi zote zinazo husiana na chuma kwenye miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia mafundi wake wa sekta tofauti.