Hospitali ya rufaa Alkafeel imewapunguzia gharama za matibabu familia za mashahidi kwa asilimia %25.

Maoni katika picha
Hospitali ya Rufaa Alkafeel haijawahi kuacha kuwasaidia watu wenye kipato cha kidogo na familia za mashahidi kwa kuwapa punguzo la bei au kuwatibu bure, hivi karibuni hospitali imewapunguzia gharama za matibabu kwa asilimia %25.

Mkuu wa taasisi ya Mashahidi mjini Karbala Ustadh Ali Haadi amekiri kupata taarifa ya punguzo la gharama za matibabu kwa familia za mashahidi katika hospitali ya rufaa Alkafeel kwa asilimia %25.

Akabainisha kua: “Punguzo linahusu makundi yote katika mikoa yote” akasema: “Namna ya utekelezaji wa punguzo hilo, mgonjwa atapewa utambulisho maalum na kitengo maalum ili kumuingiza katika punguzo hilo”.

Mkuu wa kitengo cha matibabu na bima katika hospitali ya rufaa Alkafeel Ustadh Abbasi Fadhili Hamadi amesema kua: “Makubaliano ya punguzo hili yalifikiwa baada ya ziara ya kwanza iliyo fanywa na wajumbe wa taasisi hiyo wakiongozwa na Ardawi katika hospitali hii, wakakutana na mkuu wa hospitali Dokta Jaasim Ibrahimi na kujadiliana kuhusu punguzo la gharama za matibabu”.

Fahamu kua Hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu bado inaendelea kutekeleza ratiba zake za kibinaadamu kwa kuzisaidia familia za mashahidi na za wenye kipato kidogo kutoka miji tofauti ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: